HUKUTAKIWA KUANZA HIVYO

 
Sikuwa na sababu ya kuandika hiki ila imenibidi baada ya kuona kuna umuhimu wa kuwakumbusha vijana wenzangu wale walioko kwenye mahusiano na zaidi kwa wale ambao bado hawajaingia kwenye safari hii nzuri kuelekea ndoa. Kumekuwa na upotoshaji sana kwa watu wanaoingia kwenye mahusiano ,sijui wanapata wapi hayo maarifa,yawezekana ni waalimu wao wa mahusiano ambao wanajali sana ustawi wa mwili kuliko kiroho cha mtu. Tena wengine wanasema hupaswi kuanzisha mahusiano mpaka umelijua kusudi la Mungu kwako,hahahahahah! Vipi kuhusu Ibrahim,Daudi na wengine waliooa kabla.
~kwa ufahamu wangu kusudi la Mungu halitafutwi bali linajifunua lenyewe katika maisha yako
~ Usidanganyike kihivyo wengine wapo kwa ajili ya kuonyesha ufundi kwamba waonekane wanajua kufundisha sana lakini ukifuatilia katika kuoa kwao nao hawakuoa wakiwa tayari wanajua kama wanavyokulazimisha wewe leo. Paulo anawaambia watu ,"ni heri kuoa kuliko kuwaka tamaa", nikuulize swali paulo hakuwa anaelewa umuhimu wa kufahamu umuhimu wa kulijua kusudi la Mungu?
 Mahali pengine pameandikwa *wale aliowajua tangu asili akawaita..........* sitaki ninukuu kama kilivyoandikwa ila soma ~warumi 8:29-30~ Kwa hiyo kutokana na mafundisho hayo watu wengine wameogopa kuingia kwenye mahusiano kwa sababu hawalijui kusudi lao,niseme tena kusudi la Mungu linakuja kwangu kama *divine appointment*mtazame Mussa mpaka anakutana na kusudi la Mungu kwanza hakuwa anafahamu hivyo ilikuja kama divine appointment na vilevile alikuwa amekwisha oa tayari so i dont see any useful point on that.
 Sasa kama umeanza mahusiano kwa mtindo huu ninaokwenda kukwambia ujue kabisa *hukupswa kuanza hivyo* na kama hukuanza hivi sikwambii uvunje ila usalama wako ni mdogo kuliko maelezo ninayoweza kuyatoa na kama hujaanza basi ~basi hupaswi kuanza hivi~
; Kuanzisha mahusiano kimyakimya
 Kwanini si vizuri kuanzisha kimyakimya?; ·
Waweza jikuta umeanzisha mahusiano na ndugu yako halafu hamfahamiani halafu mnakaa mpaka kipindi mlichopangiana kujitambulisha kwa wazazi ghafla mnaambiwa nyinyi ndugu,hapo mnakuwa mmepotezeana muda na tayari mioyo imeshashibana,kisa kama hiki kilimkuta dada fulani ambaye ni rafiki yangu. ·

Waweza jikuta unakosa kibali cha wazazi kwani mtoto mwenye busara lazima awe na mzazi mmoja ambaye anaweza kumwambia chochote na wakashauriana ,kwa kufanya hivi mzazi anajisikia kuheshimiwa na utakuwa na mtu anayekuombea ili ufikie mwisho mzuri.
·
Unapata ujasiri na kuamini kwamba hauko single tena hivyo na huwezi kuishi kama hauna mtu ambaye unampango wa kuwa naye,utajibidiisha kufanya yapasayo kuupendeza moyo wa mwenza wako na kuboresha future yenu.

Hasara kubwa ya kuanzisha mahusiano kimyakimya au kuyafanya yawe siri ni;

 Kukosa kutambulishwa au hata kutajwa mbele ya rafiki zake mpenzio.

Ni ngumu kufika mwisho,naomba nieleweke ninaposema ngumu si kwamba haiwezekani hapana! Inawezekana kufika mwisho lakini kwa kupambana sana.
 Nisiseme mengi lakini kama ni mahusiano ya kweli kwanini yawe siri ,kwanini hakuna hata mtu wa kwenu anayekushauri au mzazi wa kiroho anayekushauri na kukuombea rafiki eeeeeeh!,aseeee usifanye hivyo hata kama anakuomba hebu tafuta kujiridhisha kwa kina kabla hujakubaliana nae.

 Laban Nzelela

Comments