Tangu umeanza kusikia habari uongozi wa demokrasia yawezekana hukujua hili,maana kiukweli  hakuna uongozi wa kidemokrasia ambao hauna tabia ya mabavu ndani yake na kama kungekuwa hakuna mabavu kidogo yanatumika kwenye maamuzi basi kungekuwa na matumizi makubwa ya muda katika kufanya maamuzi.
Wewe mwenyewe ni shahidi kuna mambo yalishajadiliwa kwenye vikao mbalimbali kuanzia ngazi mtaa mpaka taifa cha ajabu yaliyopingwa ndo hayo hayo yakapitishwa na watu wakakaa kimya.
Wapinzani wanaweza wakafanya uzuri mwingi kuonyesha kazi yao ya kuonyesha madhaifu  ya serikali iliyoko madarakani lakini waseiwe na upinzani wa kweli,mimi naamini hakuna mpinzani wa kweli kama yule anayepinga vitendo visivyokubalika ingali ni mmojawapo kati ya serikali tawala.
Pata nafasi yako,fanya yako kwa uzuri wa taifa lako.

Comments