HAPO NDIPO UNAPOTOFAUTIANA NA MWENZAKO
Kioo huwa hakisemi uongo ila huwa
kinaongeza sifa ambazo wakati mwingine huwa haunazo,usahihi au upungufu wa
taarifa hutegemea aina ya kioo maana kuna vingine huonyesha mkono wa kushoto
uko kulia na
wa kulia uko kushoto.
Maisha ya wengine hawayezi kuwa
kioo chenye taarifa sahihi kwako ila hukufanya ubadilike au uongeze kasi ya ufanyaji wa mambo yako,,,,,ila dah tofauti yako na mwenzio iko hapa.........................
Wakati wewe unapiga hesabu ya
wapi utapata elfu ishirini ili ikamilishe laki moja kuna mwenzio tena
yawezekana ni mshirika wako au ni mtu unayemuongoza kanisani au ofisini kwako
huyo mwenzako anawaza atawasaidiaje watu wenye shida kwa kidogo alichonacho.
Wewe unapoomba Mungu akubariki
uwe na nyumba,gari,familia nzuri ili uishi kama uko paradiso,wakitajwa wenye
nazo na wewe uwepo tena unafunga na kufunga lakini mwenzio huyo jirani yako
yeye aombapo huwakumbuka wenye uhitaji kama mayatima,wazee,wajane na walemavu
tena huumia akiona hana namna ya kumsaidia hivyo muda wa kujiombea yeye hutumia
kuwaombea wengine tena kwa machozi eeeeeeeeh! Mungu.
Tena huwa unanishangaza kwani
kutoa kwako sadaka ni kama yule mtu akopeshaye maana hutaka sadaka yako irudi
tena na zaidi , mmmmmh Fulani hakuelewagi pia lile neno unalopenda kulitumia
kuwa Bwana atakupa vya kujaa na kushindiliwa hivyo sadaka yako isiwe bure
loooooh! Unajua unatofautiana wapi na mwenzio,,,yeye hutoa kw a moyo wa
kumshukuru Mungu na wala hatarajii Mungu ampe eti kwa kuwa ametoa bali hutoa
kwa kuwa anampa aliyempa.Sasa aliyetoa unamkopesha kwa riba kweli!!! HAPO NDIPO UNAPOTOFAUTIANA NA MWENZAKO
Unalalamika hakuna anayekujali
kanisani kwako hata ofisini kwako,na muda wa ibada unapoisha wewe
unaondoka tu hata husalimiani na watu,muda wa kazi ukiisha unaondoka hata huagi
wenzio,kwenye masuala yanayotaka umoja wewe ni wa kwanza kukosoa,na kutoa
mapendekezo mazuri ambayo hata huyafanyii kazi wewe ni kubwabwanya
tu,,,,,,mwenzako sasa wakati unapoondoka yeye anabaki na kusalimiana na watu na
kuagana nao,nani ajaliwe kati ya wewe na mwenzio,
Been unique is not avoiding others but by being blessings to others makes
you to be unique and useful and that is possible when you associate with
others.
Tena hili nalo limekufanya
utofautiane na wengine si kwamba unachanua bali unafifia na kinachokufifilisha
ni kwa sababu hujui unachotakiwa kukifanya kama ndo kitu ulichozaliwa ili
ukifanye hivyo unaishi maisha ya watu wakati mwenzio anaishi kama alivyo ili
akiinuka awe ameinuka moja kwa moja.
Huyu mwenzio si mkeo wala si mumeo bali ni kila anayekuzunguka katika jamii yako.
Nitaendelea kukwambia jinsi unavyotofautiana na mwenzako.
Bro.laban Nzelela
@ftfteam leader
Comments
Post a Comment