KUWA KAMA ULIMBO KWA MWENZA WAKO




KUWA KAMA ULIMBO KWA MWENZA WAKO
Nianze kwa kusema sifa ya ulimbo.
Ulimbo hukamata kile kitu ambacho hakijazidi uwezo wake wa kunasa, kwa mfano ulimbo hauwezi kumnasa tembo kwani tembo uwezo wake ni mkubwa kuliko nguvu ya ulimbo.
Wakati nilipokuwa nakua miaka ya tisini huko nilikuwa nikitega ndege kwa ulimbo kwa kutumia kijiti ambacho nilikuwa nakichomeka karibu na sehemu yenye maji ambako huwa ndege walikuwa wanakunywa maji na alipokuwa ndege ametua kwenye hicho kijiti basi hakuweza kujinasua kwenye ulimbo.
Mfano huu usikuchanganye sana ila kila upendo wa wawili hudumu ikiwa nguvu yao ya kuvutana katika mioyo yao vimetoshana yaani mmoja ambaye amefanikiwa kunasa moyo wa mwenzie. 
Kwanini uwe kama ulimbo kwa mpenzio??
Kuna sababu nyingi zinazokufanya uwe kama ulimbo kwa mfano huu;
A: Ulimbo huwa hausahau ikiwa kuna windo limenaswa kupitia huo ulimbo.
Ukiwa na sifa hii,
1: Hutaweza kumsahau mwenza wako
2: Hutaweza kumshusha thamani yaani upendo wake kwako hautakuwa kitu cha kawaida kwako.
B: Ulimbo hupoteza nguvu kadri ya windo linavyojitahidi kujinasua.
It is very true when you try hard to push away your lover from you he/she gets tired and loose the first love when you agreed to be together and finally get married.
This can separate you from your lover.

C: ulimbo hupata nguvu zaidi unapopigwa na jua.
Kama utazikubali changamoto basi changamoto hizo zitakufanya kuwa mke au mume bora baadae,na endapo utaonyesha kuzikimbia basi ni sawa na ulimbo kuutia michanga na matope mengi ambayo yatapunguza uwezo wa kukaa na windo.
Simaanishi ulipo ni lazima uendelee kuwepo bali itazame tena thamani ya moyo ulioamua kukupenda na kukubali kuacha wengine na hata wakati mwingine moyo huo umesitisha kusoma au kuanzisha mradi Fulani ili mradi tu mfikie kuoana kwanza hakafu hiyo mipango itaendelea.
Nilikua sifahamu maana ya kifungu kinachosema "upendo hautafuti mambo yake yenyewe" ziko sifa kibao pale ukizisoma waweza ukaona kama ni hadithi tu ila nilikutana na mama mmoja ambae alinambia kuwa yeye aliacha kusoma kwa sababu ya mchumba wake ambae alitakiwa aoe haraka iwezekanavyo hivyo akaacha kuendelea na masomo na kisha akaolewa na mpaka sasa ninavyoandika ana watoto wanne na wa kwanza anaenda chuo,sambamba na hayo na yeye ana masters.
My words to you if you have someone loving you know this he is just not there because of your beauty or your handsome but he is there for a purpose, never let him be alone in his darkest hour or her in her miserable situation. Just stick there, he is sacrificing for you, so pray for her or him.
Ni ukweli usiopingika hakuna kati yenu mwenye moyo wa chuma.

Bro. Laban Nzelela
FTF team leader.
    Dedicated to my dear future wife and my dear readers.


 

Comments