MAHUSIANO: KWANINI USILIE UNAPOPIGWA KIBUTI



Nikisema hili neno kibuti japo si rasmi lakini wengi tunalielewa,tena ndugu yangu Bedon Dickson hili neno analifahamu mno na analitumia sana nyakati anapowasilisha mada hizi za kuacha au kuachwa.
Kibuti linamaanisha ni kuvunjika kwa uhusiano bila makubaliano ya wahusika,,unajua si kila wanaoachana basi hugombana au huachana kimyakimya,hapana kuna wengine hukubali kuachana kwa moyo safi bila kuweka kinyongo kwa mwenzako.kuna mazingira hutokea na watu huamua kuachana kwa taarifa na tena na kuombeana wataombeana na kutakia mema huko ambako kila mmoja atakwenda.
Lakini si hili neno kibuti,ukisikia Fulani kapigwa kibuti huwa ni aibu,tena unaonekana wewe huwezi aseeeee,kama una watani wako basi siku hiyo itakuwa ni kiyama cha furaha yako maana malaika wa huzuni na aibu atakuwa amekushikilia,
,ubaya uko hapa apigaye kibuti huonekana shujaa kuliko yule aliyepigwa kibuti maana kwake ataona ametoka kwenye tanuru.
Kibuti hakihitaji maelewano,unaweza pigiwa simu tu siku hiyo tena wewe bila kujua ukaanza,,; hello,baby umenikumbuka asubuhi, miss you, love you,, enheee nambie mpenzi wa moyo (ukijisikia kupenda mno)
Weeeeeeee !!!angalia jibu hilo sasa
;aaaaah safi tu,(huku amekunja USO),,mi naona tuachane tu na kuanzia leo usinipigie simu na namba zangu futa kabisa.
Daaaaaaaah! tena nimekumbuka mimi nilishapigiwa simu nikaambiwa hivyo sema sikua kweli katika mahusiano na huyo binti ila alihisi natamani kuwa nae na nilipojaribu kumwambia Mimi ni kama rafiki hakunielewa mpaka alipopata mbadala wa mvulana mwingine ndo akanipigia hiyo simu.
Kibuti kinauma,ni kweli kinakushushia heshima lakini wakati mwingine kinakufundisha na kukukomaza.
Kwanini usilie unapopigwa kibuti???????????
Hii si rahisi hebu imeze kama dawa chungu vile ili ikusaidie huko ndani.
A: Hukuendana na tamaa ya moyo wake
Si kama utakuwa unajifariji hapana ila zingatia hili,"kila mke mwema alitokana na mwanamke aliyekuwa na sifa za kuwa mke na si kila mwanamke aliyezaliwa na mwanamke aweza kuwa mke mwema kwako"
Vivyo hivyo,"wanaume ni wengi kuliko maelezo lakini mume mwema ni yule atakayekubali kuwa mume wa mtu na wala si Wa kijiji"
Labda alikuja kwako kwa sababu ulionekana ni aina ile aliyoitaka lakini alipogundua hapa sipo nitachemka ikabidi aombe poooo!!!, she/he thought that you are just a sexy machine and not a man/woman with a quality of been married.
B: Ulimuomba Mungu akupe mwema na huyo hakuwa mwema ndo maana kaondoka.
Ukielewa hapa hautajuta hata kama muda umepoteza mshukuru Mungu acha kukunja uso kama Mzee,acha kuharibu uso wako kwa machozi yasiyo na tija, au umesahau aombaye mkate hapewi jiwe bali hupata alichoomba??
C: Unastahili zaidi kuliko alivyofikiri.
Nafikiri ulishawahi kusikia baadhi ya watu wanasema mi siwezi kuwa na mtu Fulani kwa sababu anaonekana yeye ni matawi ya juu,,,,huo ni msemo ambao huwafanya watu wajitoe kwenye kinyang'anyiro hicho.
Simaanishi pesa hapana angalia hadithi hii,"kulikuwa na kijana mmoja ambaye alivutiwa na binti Fulani ,hivyo akapanga namna ya kuwa karibu ili aweze kumnasa bahati nzuri alifanikiwa kuwa karibu na binti tena ni ule ukaribu wa mtu na mpenziwe.lakini lengo la kijana lilikuwa ni kumtumia na akishamtumia basi aachane nae.
Kadri ya ukaribu ulivyozidi na mahaba kuongezeka kijana akaanza kusikia hukumu moyoni mwake kwani yeye hakuwa na mpango wa penzi la dhati bali ni wizi kisha kibuti lakini kwa kuwa msichana alionyesha penzi la dhati ,,jamaa akashindwa kuuficha ukweli akamwambia kiukweli nilipokuona nilikutamani na nikapanga nikuumize na mbinu zangu zimefanikiwa bado moja tu lakini hilo moja siwezi kulifanya na naomba tusifike mbali tuwe rafiki tu,."
Anapogundua unastahili zaidi ya vile alivyokuona anakosa ujasiri wa kuendelea hivyo anaruka na kuliacha gari katika mwendo.
Pole kama yamekukuta na kama hayajakukuta elewa haya mapema maana moyo wa mtu ni kichaka.

#ftfteam

Comments