Unapokuwa
umeamua kuwaacha wote na kuamua kummamini mmoja tu ambaye huyo mnaweza mkafanya
maisha
Mnaweza
kuunganisha si yai nabegu ili kupata watoto tu Bali hata utafutaji wa maisha
ili kiwa na future iliyo nzuri.
Ujue japo huwa tunasemaga
akiniacha nitatafuta mwingine mioyoni mwetu huwa tunamaana tofauti na maneno,,.uhusiano
wowote unapovunjika huacha maumivu hata kama ulikuwa ni wa kirafiki tu.
Mawasiliano
ni jambo muhimu mno kwa kila nyanja ya maisha yetu.
Mawasiliano
si kwa kutumia simu bali ni zaidi ya kupigiana simu au kutumiana jumbe fupi.
Mawasiliano ni mahusiano kauli
uzitoazo huonyesha dhahiri mahusiano yako yakoje na watu au mtu unayewasiliana
naye ,ukiongea kauli za kuumiza zinazosababisha maumivu ni dhahiri hivyo ndo
namna mnavyohusiana.
Uti wa mgongo wa mahusiano ni
mawasiliano na kila eneo au nyanja ya maisha yako kauli safi zisizoumiza
zinahitajika ndo paulo katika nyaraka za timotheo anasema uwe kielelezo na
anataja neno katika usemi.
Endapo
yatavurugwa au hayatakuwa na kutiliwa mkazo basi kuna hatari kubwa
yakaharibiwa,kufa au bora liende.
Wewe
mwenyewe ni shahidi wakati ujenzi wa mnara wa Babeli kilichowabeba hata kufikia
hatua ile ilikua ni mawasiliano.
Yaani lugha rafiki ndo iliwafanya
wawe wamoja mpaka Mungu akaamua kuvuruga usemi wao.
Kwenye biashara yako kosa lugha
rafiki kwa wateja wako hapo ndo utakapojua kwanini mwanga wa mwezi ni muhimu
lakini haukaushi mazao.
Kwenye familia lugha ikichafuka
hiyo sio familia ni genge la wababe.
Nchi ikikosa usemi unaoeleweka
basi ujue hata kama mti wenye mwiba si rahisi kuupanda utageuka mwembe tu.
Kanisani usemi ukichafuka ndo
utafahamu imani ya watu kwa Mungu wao.
Kadhalika katika mahusiano ya
urafiki kuelekea uchumba hata ndoa inategemea sana lugha rafiki, lugha rafiki
ni lugha isiyoumiza upande wowote.
Unaweza kuchagua mwenyewe ipi
itakufaa na ukaonekana ni wa busara mbele ya nwenzi wako.
Uchaguzi ni wako kuchukua kiatu
cha wazi au cha kufunika,kutangaza mambo yenu ya mahusiano au kuyatafutia
ufumbuzi wako mwenyewe.
Uchumba,urafiki au ndoa
inayokosa mtu confidant ni hatari sana
Mume anahitaji mke
confidant,vivyo hivyo mke anahitaji mume confidant yaani mwenye kifua.
Lugha zenye chembechembe za
kuumiza husababisha utengano wa mioyo kati ya wapenzi.
Kuna kauli au maneno ambayo
unatakiwa kuwa makini nayo wakati yanatumika au yaepukwe ili kuepusha
kuumizana.
Kauli hizi huonyesha muyumbo au
kifo cha mahusiano
Tuziangalie kauli sita za
kuepukwa ili kuwa na mahusiano bora.
Hebu zitazame kwa umakini
hizi kauli halafu utanambia hata kama zinaonekana ni za kawaida lakini zimebeba
sumu Kali inayoweza kuleta giza na ukungu wa huzuni katika mahusiano yetu
Kila mtu anapenda afurahie
na ajisikie ni yeye tu katika dunia hii tena kama ni mkeo ndani
ya ndoa hata ukijaza account yako ya insta au Facebook kwa kumsifia sitashangaa
maana hiyo ni lugha tamu.
Weka hata kwenye wallpaper yako
picha ya mama mtarajiwa au baba,,save jina zuri hata akijaribu kujibipu anaona
jina my cute,my queen, wala si my headache
1: Kama ni hivyo mi nitashindwa.
Kauli hii huweza kujitokeza
endapo kuna mmoja kati ya wapendanao anaonekana kutoeleweka,au mmoja anashindwa
kumwamini mwenzie hivyo hutishia kuvunja uhusiano
Utasikia tabia zako sizielewi
elewi,mbona hufanyi kama tulivyokubaliana kama ni hivyo mi nitashindwa na
tutaachana.
Hakuna jambo baya kumtishia
mwenzio ikiwa tayari ameshajikita kwako,hii huzaa uchungu,hujenga maumivu kwa
mwenza wako.
Mimi naamini kuna maneno
yanaweza tumika kama mbadala ya kauli kwa mfano tabia yako haipendezi hivyo
iache.
Na si kutishia kuvunja mahusiano
pasipo kuzungumza kipi ni kibaya kati yenu.
Na hata kama itatokea
mmevunja mahusiano ya uchumba wenu itakua ni kwa sababu zenye mashiko labda
mkioana si rahisi kupata mtoto kutokana na sababu za kibailojia,na
hapa ina maana kila mmoja atajua kwanini mnaachana na kuridhiana kutoana
mioyoni kabisa.
Najua urafiki au uchumba si ndoa kama unaona hauendani au unaona huyu si mtu sahihi na labda ulikurupuka kwenye kuamua kutokana na labda ulichokuwa umepitia kilifanya usifikiri kwa makini ila ulimpa nafasi ili kuziba pengo na sasa unajiona umerudi kwenye ufahamu wako,ongea kwa uzuri naamini suluhisho litapatikana .
Najua urafiki au uchumba si ndoa kama unaona hauendani au unaona huyu si mtu sahihi na labda ulikurupuka kwenye kuamua kutokana na labda ulichokuwa umepitia kilifanya usifikiri kwa makini ila ulimpa nafasi ili kuziba pengo na sasa unajiona umerudi kwenye ufahamu wako,ongea kwa uzuri naamini suluhisho litapatikana .
kuliko kutishia kwa maana
unajuta kuwa nae na unamtafutia sababu ya kuachana nae,sababu unayo tayari tell
the truth.
2: kwa sasa tusizungumzie mahusiano
Yaani
mko kwenye mahusiano tayari lakini mmoja wenu anasema tusizungumzie mahusiano
kwa sasa.
Why;
shule imebana,kazi imebana sana
Hivyo nashindwa
kugawa muda kati ya kazi na mahusiano kwa hiyo tafadhali tuache kwanza.
"Kuna rafiki yangu alinifuata kipindi tuko chuo mimi mwaka wa pili na yeye wa kwanza na kunambia kwamba anamsichana amempenda sana hivyo nimshauri kama vipi awe nae.Baadae ya kumuuliza maswali kadhaa nikamwambia sawa kuwa nae.
Lakini baada ya msichana huyo kumaliza chuo na jamaa akawa bado ndipo akamwambia', kwa sasa tusizungumzie mahusiano'"
"Kuna rafiki yangu alinifuata kipindi tuko chuo mimi mwaka wa pili na yeye wa kwanza na kunambia kwamba anamsichana amempenda sana hivyo nimshauri kama vipi awe nae.Baadae ya kumuuliza maswali kadhaa nikamwambia sawa kuwa nae.
Lakini baada ya msichana huyo kumaliza chuo na jamaa akawa bado ndipo akamwambia', kwa sasa tusizungumzie mahusiano'"
Kauli hii ni mwanzo mzuri wa
kuumiza moyo wa mtu na pia ni njia isiyo na miiba iendayo kwenye kuvunja
mahusiano.
Hapa yawezekana amezungumza kwa
ufahamu wake mdogo tu na wala hana mawazo ya kuvunja,,,au ana mawazo ya
kumaanisha kuvunja hivyo anatafuta mbinu ya kukuweka kwenye mazingira ya
kukuacha hivyo unaandaliwa kisaikolojia ili akichomoka uwe umeshazoea.
Kuna watu wako bize na bado wana
jenga mahusiano yao vizuri tu.
3: Sijui Itakuje?
Hii
kwetu wanaume kwanza lazima uelewe hupati mke eti kwa kuwa unahela ,,pesa
hazimfanyi mwanamke anayejielewa akatamani kuishi na wewe,,,
Wanawake wanapenda wanaume wanaojielewa, mwanaume anayeulizwa na kujibu kama kazaliwa na jibu hilo,sio unaulizwa sherehe itakuaje?,unasema hujui,,kaaaah!!!
Wanawake wanapenda wanaume wanaojielewa, mwanaume anayeulizwa na kujibu kama kazaliwa na jibu hilo,sio unaulizwa sherehe itakuaje?,unasema hujui,,kaaaah!!!
You
have to straight know that you will soon be the head of the family or you are
in already so make your woman been proud of u
No
matter you don't have enough for today but as long as you are bold hustling,am
sure her heart is yours.
Na wanaume
hupenda mke mwenye fikra pevu,jibu la sijui huwa linatoa sura ya mke mwema na
kuweka mke asiyejielewa.
Huleta wasiwasi kwa mwanaume
hasa mwenye malengo makubwa anapoona hufanani na yawezekana si kweli ila
unakosa umakini.
4: Umeanza kama kawaida yako
Hapa huonyesha moyo wa mmoja
umekuwa sehemu ya kuhifadhia vitu vibovu.
Mfano rahisi pita kwenye dampo
na ukakuta hali ya hewa safi,kisha chukua kijiti na fukua kwenye uchafu hapo harufu
itakayotoka hapo ni hatari.
Ndivyo moyo wa mpenzi
anayehesabu makosa hivyo ukikosa haanzi na la leo bali la mwezi uliopita mpaka
afike la leo si chini ya lisaa limoja ni lawama tu.
Hii mbaya mno kwani huonyesha
uwezo hafifu wa kusamehe na hivyo kumfanya mwenzio ajisikie ni mkosaji
asiyestahili kusamehewa.
Hata kama uko kwenye ndoa tayari
chunga sana hili eneo utatia tope kwenye kiti cha harusini halafu ndiwe
unayetakiwa kutoa nasaha ,utainukaje wakati ushachafuka aseeee.
Kila mwenye kidonda anajua kukilinda ili kisisumbuliwe na nzi au kutoneshwa iweje wewe usiweze kulinda mahusiano yako.
Kila mwenye kidonda anajua kukilinda ili kisisumbuliwe na nzi au kutoneshwa iweje wewe usiweze kulinda mahusiano yako.
5:"Kama vipi basi",
Hii husemwa si kwa lengo la
kuridhika bali ni kama kero hivyo unaamua bora liende lakini si kwa uzuri.
Hii inaleta kutu kabisa kwenye
mahusiano.
6: Lazima Asikie Uchungu wa Mke’
Msichana anasikika akijisemea
kwa rafikize kwamba ili mchumba wake aone uchungu wa kuoa basi inabidi
agharamike katika kutoa mahari ndefu.
Mbaya zaidi katika vimazungumzo
vya kubadilishana mawazo na mtarajiwa wake anaanza tena,"mimi ni mwanamke
mzuri,na nimesoma hivyo mahari yake hapa inabidi ujipange,na ninavyojua wazazi
wangu na hata kama ningekuwa mimi ndo mzazi mwanangu angeolewa kwa
gharama".
Eeeeh! Ni vyema lakini hata
ikisemwa kwa utani bado inapenya kwani huo si utani bali ni mzaha na mzaha
hutumbua jipu.
Kama wewe umesoma hivyo
unatakiwa uposwe kwa pesa ndefu ungeolewa na elimu yako kama inawezekana.
Kama msichana unajielewa hii si
kauli ya kuzungumza popote pale ulipo.
Bro.labannzelela.
Founder ftf.
Founder ftf.
Comments
Post a Comment