NENO LA MUNGU: KIELELEZO CHAKO KIKO WAPI?





SOMO:  KIELELEZO CHAKO KIKO WAPI?
NA: Bro Laban Nzelela
Sehemu ya kwanza.
Maandiko yamenena hivi,*mtu yeyote asiudharau ujana wako Bali uwe kielelezo........" 
Mi hata sitaki kuzunguka ila naomba niseme hili,kwa hali tuliyonayo sasa hasa kanisa au waaminio wokovu (kuzaliwa Mara ya pili), ni hali ambayo imechangamka mno tofauti na zamani maana vijana tumekuwa na mwamko wa kumtumikia Mungu tena tunajitoa hasa.

·         Miaka ya nyuma ilikua nadra kukuta vijana wamependeza tena wanamikato ya hataree wanachapa injili lakini kwa sasa tumevunja record maana idadi imeongezeka na watu wamepanda mori(sio ile ya kimasai),yaani wameamka.
·         Mbali na kuwa wimbi la vijana wanaokimbilia kwenye huduma linaongezeka lakini mvuto Wa huduma nao unapungua,heshima na maadili ya kikristo hawaeleweki ni kama mlevi ambaye akiwa hajanywa huwezi elewa kama ni mlevi ila akinywa ni hatareee.
·         Labda mwenzangu waweza ukawa na jibu? eeeeeh! Kama unalo tusaidiane kukumbushana.
Yaani ile hofu na heshima iliyotajwa na Yesu kuwa tutaipata tukimtumikia Mungu bado iko mbali na si rahisi kuifikia,Napojiuliza naona kuwa vijana wengi tunapoteza sura na ladha ya wokovu hata kama tunakiri tunamtumikia Mungu aliye hai .
·         Upentecoste naufananisha na mbuzi anayefahamu mahali ambako kuna maji au mnyama yeyote wa kufugwa pindi anaposikia kiu hata kama utamzuia ni lazima ataenda na kunywa, ndivyo tulivyo sas a *wenyeji umezidi sana kiasi kwamba tunaona kawaida*.
·         Ufunuo aliposema mmemkaribisha mbele tena mmempa kiti cha mbele akakaa,!!! najiuliza alikuwa anamaana gani?????.
·         Okay tufanye hivi kwa Leo wewe kama ni kijana na unatumika jitahidi usiwe kila kitu, kuwa na mtu aliyekutangulia tena itafaa awe wa zamani kidogo ili ujifunze maadili ya kiktisto hii itakuwa rahisi kwani utakapokuwa unaongezeka katika viwango vya utumishi na malaumu nayo yatakuwa yanapungua.
·         Usidharau hili tena unapoambiwa hili vazi sio tii,namna ya utumishi wako kuna vitu punguza kubali kwani *kabla ya huduma unayotoa maisha yako ni huduma tosha*,mwana mzuri ni yule anayekubali maonyo na mafundisho.
Kielelezo kimepotelea wapi?
Hapa ndo shida sasa,kama hujajua unatatizo basi ni ngumu kulitatua tatizo.
Kama huamini muulize daktari ambaye anahudumia mgonjwa asiye na uwezo wa kuzungumza,hiyo diagnosis daktari anapata kazi sana kumwandikia mgonjwa wa namna hiyo.
Hata mwana wa nabii aliyedondosha shoka aliulizwa na Elisha limedondokea wapi?, kujua tatizo na chanzo cha tatizo ni robo tatu ya suluhisho la tatizo lako.
Kuna mambo lazima uwe makini nayo hasa tunapokusanyika vijana katika makusanyiko mbalimbali,kwani wengine hukisanyika kwa lengo tofauti na lile lililowakusanya kulingana Yale wanayoyatamani.

HAPA NDIPO ULIPOPOTEZA KIELELEZO CHAKO.
1.      Makusanyiko ya vijana tupu.
Hata mwana wa suleimani alipopuuza ushauri wa wazee na kuamua kuukubali wa vijana wenzie tunaona madhara aliyoyapata.
Waliotangulia ni hazina yetu hata kama wanaonekana kuishiwa mbinu,samweli hakumdharau Mzee Eli hata kama ilionekana Eli ameshachoka kiroho na kimwili hata Mara baada ya kuambiwa na Mungu bado alimheshimu.
Kwenye makusanyiko mengi ya vijana usipokuwa makini unaweza kupoteza kielelezo chako maana wote mko kwenye hatua moja ya ujana.
Mfano rahisi tu usiyohitaji shule ni kwamba asiyeoa hatakiwi kuombwa ushauri na mtu anayetaka kuoa,unataka kuoa tafuta watu ambao wamekaa kwenye ndoa angalau miaka mitano na kuendelea.
Vijana wengi wanatumia uzoefu wa miaka miwili au mmoja katika huduma halafu wanajiona wamekua.
2.      UNAJILEA AU UNALELEWA (you got a spiritual father?)
Kama huna baba wa kiroho nakuhakikishia utayumba tu,kwani baba wa kiroho yupo kukuongoza na kukufundisha ili kuufikilia wito wako lakini kabla hujafikia huko ni lazima ulelewe vizuri.
Nikwambie siri hii, baba wa kiroho huwa hasemi ndio kwa kila unalofanya.
Baba wa kiroho si mshauri wako tu hapaba bali anawajibika katika kufanikiwa na kushindwa kwako.
Wengi wanawashauri na wala si baba kiroho,japo wao wanaamini ni baba zao kiroho.


Note; If you are spiritual father all he can say is yes then he is not your spiritual father, he is just encouraging you and once you fail he will not be answerable.

3.      KIPI CHA KWANZA KATI YA MUNGU NA HUDUMA KWAKO.
Kuna mtu aliwahi kusema hivi,"nafasi yako au cheo chako kanisani au kwenye vikundi vya kanisa havina nafasi katika mahusiano yako na Mungu"
Kwa kusema hivyo si kama hakutambua umuhimu wako katika nafasi hiyo bali alitaka tutofautishe maisha yetu na Mungu na Maisha yetu katika vyeo vya kwenye huduma,unaweza ukaitwa majina mengi kwenye vikundi unavyoongoza lakini hayo hayasaidii kuboresha uhusiano wako na Mungu.
Ukikosea kwenye kipi kianze kati ya Mungu na huduma basi kielelezo ni ngumu kukipata.

4.      KUCHANGANYA WAGONJWA.
Kinachotoa umakini na umahiri kwa daktari yeyote ni kuchanganya matibabu kwa wagonjwa,wewe mwenyewe ni shahidi kuna oparesheni zilikosewaga baada ya mgonjwa aliyetakiwa kupasuliwa goti akapasuliwa kichwa na yule wa kichwa akapasuliwa goti,kilichotokea baadae ndicho kiliwashusha thamani madaktari.
Wewe ni kijana na unafundisha sana vijana mpaka imefikia unatumia lugha zile za vijana,hapo si shida maana ndo mahala pake..
Tatizo linakuja unapochanganyiwa wagonjwa yaani watu wa kuwahudumia unapewa kanisa zima kwa mfano na kwa kuwa umezoea vijana jitahidi usiwape kanisa dozi za vijana endapo utachanganya madawa basi ujue unaleta madhara.
You are not qualified so God is just trying to prone you.

Itaendelea………..
FTF team  leader


Comments

Post a Comment