KUNA FAIDA ZA KUWA KARIBU NA MTU ALIYE NA MUNGU WA KWELI
NA MWL: COSMAS MALANDO
Maisha ya mwanadamu ili yafanikiwe yanahitaji kutembea na watu sahihi wanaweza kumsaidia katika namna mbalimbali.
Jambo la muhimu katika maisha yetu ni kumfahamu Mungu kibinafsi
Ukimfahamu Mungu binafsi yeye anatembea na wewe, anakuwa na wewe ataishi kwako
Luka 10: 38-42
Martha na marimu mtu na mdogo wake
Mariamu aliamua kukaa miguuni pa Yesu, alikubali kujifunza kwa Yesu
• Kukaa karibu na mtu aliye na Mungu
Yohana 11 :24
Ruthu 1 :12-17
Tunaona jinsi gani Ruthu aligundua kuwa Naomi mama yake mkwe ana Mungu wa kweli na alimng’ang’ania mpaka kikaeleweka
Ruthu 4 :13
Katika hali yake ya kutarajia kutoka kwa mkwewe Naomi Ruthu akapata Mume
Basi Ruthu akapata mume aitwaye Boazi
Mwanzo 39 :1-5
Yusufu aling’ang’ania kubakia na Mungu peke yake maana ndugu zake walimchukia, waliamua kufikiri kumuua lakini yeye alijua rafiki wa kweli ni Mungu peke yake ambaye ndiye mteteaji wake,
Ayubu 19:25 Lakini mimi najua ya kuwa mteteaji wangu yu hai, na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.
• Nyumba ya Farao hawakujua kuwa kuna faida ya kuwa na Mungu wa kweli
Yusufu alipata kibali katika nyumba ile ya mfalme, pia katika yote aliyopitia hakuhesabu changamoto alizokuwa anakutana nazo kama ni kitu kinachoweza kumzuia katika maisha yake. Alikubali kuwa na Mungu ndiyo msaada wake mkuu.
Mambo yaliyomfanya Yusufu awe na kibali
1. Alikuwa mwaminifu mbele za Mungu na wanadamu
2. Alikuwa mchapa kazi, alikuwa na bidii katika kazi.
3. Alikuwa anamcha Mungu
• Ili uwe na Mungu wa kweli inakupasa uwe mwaminifu mbele za Mungu na wanadamu
• Inakupasa uwe mtenda kazi mwenye bidi na hodari, usiwe sababu ya mambo kuharibika bali uwe sababu ya Baraka katika eneo hilo 2Tiomotheo 2:15.
• Pia sababu ya wewe kuwepo ili umche Mungu sasa kama mkristo uliyependwa na Bwana inakupasa kumcha Mungu
Umche Bwana kwa kujiepusha na uovu ili siku zako zipate kuongezeka na maaarifa yako yakue kwa kumfahamu yeye.
Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na Amani; ndivyo mema yatakavyokujia
tufikie mahali ambapo tunaweza kuwa na tukahesabiwa kuwa sisi tunaishi kwa sababu ya Kristo kama vile mtume Paulo anasema sisi mimi ninayeishi bali Kristo ndani yangu.

Enter your comment...ilikuwa baraka kwangu
ReplyDelete