Biashara yako.
Katika biashara yoyote lazima kuwe na lugha ya kibiashara kama ilivyo katika fani mbalimbali kama vile sheria,udaktari,ualimu n.k,kote kuna lugha husika.
Kutoka kwa bidhaa yako au kutokutoka hakutegemei uzuri au ubora wa bidhaa hiyo,hakutegemei elimu yako ya darasani uliyoisotea miaka kumi na kitu huko,wengi wamejikuta wakilalama eti wamelogwa na wakati kiukweli wachawi ni wao wenyewe na wamejiloga wao wenyewe.
Lugha ndio robo tatu ya maisha ya biashara yako, lugha ni mawasiliano baina ya mteja na wewe,ni muitikio wako kwa mteja,kujali kwako kwa mteja.
Lugha si maneno peke yako tu,hebu tuangalie lugha hizo ;
1:Eneo iliko biashara yako.
Hii imejikita katika uchaguzi sahihi wa eneo ulilochagua kufanyia biashara yako,kwani ukikosea kuchagua eneo la kufanyia biashara yako basi umekosa wateja,umewafukuza kabisa kabisa.
Mfano;ukitaka kufanya biashara ya mazao ni lazima utafute mahali ambako wakazi wake si wakulima au si watu wanaotegemea kilimo cha kupata chakula kwani hapo huwezi kuwapata bali waweza kuwapata.
Huwezi kufungua mgahawa eneo ambalo linazungukwa na wafanyakazi wanaotoka nyumbani asubuhi na kurudi kwao jioni ,huoni kama hutawapata maana wakirudi kwao sidhani kama watatoka kwa ajili ya kutafuta msosi.
Au kufungua duka la vifaa vya pikipiki mahali ambako hakuna wamiliki wengi wa pikipiki bali wamejaa wenye baiskeli halafu utegemee biashara ikutoe,upate faida kupitia biashara hiyo,hapana jamani eneo linaongea lenyewe kwamba hapa si penyewe.
Hivyo eneo unalochagua lazima liendane na uhitaji wa bidhaa za mahala hapo la sivyo umekosea lugha.
2:Umakini kwa mtaka huduma
Siku moja nilienda duka la dawa,cha kushangaza mhudumu wa hilo duka alinikaribisha akiwa kainamisha kichwa macho yake yakiwa kwenye screen ya simu yake akiwasiliana kwa sms, aliponikaribisha sikuitikia kabisa,mpaka alipoinua kichwa chake na kuweka simu pembeni ndipo nikamweleza ninachotaka lakini kwa kitendo cha kukaribisha mteja halafu uko umakini wako uko kwenye simu peke ni kukosa umakini,ni kudogosha mambo yenye umuhimu na kuyakuza mambo yasiyo na umuhimu.
Ni sumu inayoua haraka biashara yako kama utakosa umakini juu ya wateja wako,huwezi ukawa unaongea na simu halafu unahudumia watu,huwezi jua watu wanatafsirije juu ya hicho kitendo.
Au uko na mtu dukani mnapiga stori mpaka unaacha kuhudumia wateja unasimama kwanza kumalizia sentensi ,huo muda unaompotezea mteja utakugharimu mno.
Itaendelea...........
Comments
Post a Comment