Utulivu huashiria amani
Ukiona mtoto unapata jibu la uwepo wa wazazi hata kama wamefariki lakini alizaliwa na wazazi,na mzazi akiwepo huleta uwezekano wa mtoto.
Utulivu huashiria kuna amani,na amani huleta au huzaa utulivu.
Jambo lolote linalofanyika katika utulivu hufanya amani iendelee kuwepo na kudumu.
Kama mkristo unahitaji utulivu ,,unapotafakari katika utulivu huleta usikivu huo usikivu hukuongoza kutambua wapi urekebishe ,wapi uongeze nguvu au uendelee kwa kasi kufanya kile ufanyacho.
Sote mashahidi yule jamaa aliyesamehewa na boss wake deni na kuachiwa huru,kisha na yeye akaenda kwa anayemdai na alipoombwa msamaha alikataa kusikiliza ilihali yeye amesamehewa kilimsababishia adaiwe tena.
Mambo mengi tunaharibu wenyewe kwa sababu tumekosa utulivu,unaweza sema huna kosa kwa juujuu tu lakini utakapokaa chini na kutafakari katika utulivu Nina hakika hutaendelea kushikilia hicho unachoshikilia.
Unaweza kulaumu sana lakini endapo utashuka na kuuliza kwa utulivu utu wako wa ndani juu ya hali hiyo hakika utajua na hapo utaona kwamba hukustahili kufoka au kulaumu.
Hivi ni nani mpumbavu kati ya atakaye amani kwa mtu ambaye hataki amani na wakati huohuo anajua asiposamehe hakuna mbingu kwa ajili yake.
Utulivu ndo njia pekee itakayolinda mioyo ya wenzako,chagua utulivu,Fanya katika utulivu na ile amani na watu wote utaipat
Comments
Post a Comment