KUPENDA KWAKO KUSIKUUMIZE-Bro laban Nzelela



Dunia nzima imejaa sauti za watu,kila unapogeuka kila mtu anazungumza lake kuhusu upendo na upendo huo si mwingine bali ni wa wawili wenye maumbile tofauti ya kijinsi,yaani mwanaume na mwanamke.

Ukisikiliza sauti hizo zote kwa makini utagundua si zote zinamaanisha furaha bali kuna zingine zinalia na kuomboleza kwa maumivu waliyoyapata kutokana na neno UPENDO.
Kuna mtu aliimba na katika maneno ya wimbo wake akasema ,"kupenda pasipopendeka", nikajiuliza kumbe kuna mahali waweza penda ilihali hali wewe hupendwi? na je! upendo huu wa wapenzi wanaotaraji kuwa pamoja kwa maisha unatakiwa uweje?,wapendane wote na kuipa nafasi mioyo yao kuamua bila kuoneana huruma au kuogopa kuonekana unaringa ,ndivyo nilivyojijibu.
Siku moja nikimwambia baba yangu wa kiroho kwamba sitaruhusu kupenda kwangu kuniumize moyo,kusema hivyo nilimaanisha endapo kama nitaingia kwenye mahusiano na msichana yeyote haya yafuatayo nitazingatia

1:Sitaigiza tabia ambayo sina kwani kuna siku itanishinda na ikinishinda ndipo kibuti changu kitafuata,hivyo ili niepuke hayo nitampa nafasi ya kunizoea na kuniona tabia zangu halisi zilivyo ili kama moyo wake umekwama kwangu na ukwame.


2·sitahesabu mchumba kama ndo mke wangu tayari maana endapo nitafanya hivyo basi nitakuwa nimeuumiza moyo wangu kwa sababu mke haachwi isipokuwa mchumba waweza badilisha.Wengi wako hapa wanang'ang'ana mahali ambako hawana furaha lakini bado wako hapohapo.


3.Nitasikiliza moyo wa mwenzangu unasemaje na kama kuna badiliko lolote mbali na makubaliano yetu basi niweze kulipokea na isiwe kwangu kulazimisha.

"Si rahisi kujua kwanini unapendwa kuliko kujua kwanini unapenda" Nini namaanisha ,maana yangu hapa ni kwamba usijaribu kubadilisha mtindo wako wa maisha hasa kwa kuongezea mambo ambayo hukuwa nayo wakati ukiwa single*.

Laban Nzelela
0656574760
Instagram P.nzerol.

Comments