HATARI ILIYOPO MATUMIZI YA BIBLIA ZA SOFTWARE




HATARI ILIYOPO KATIKA MATUMIZI YA BIBLIA ZA MITANDAONI (SOFTWARE)
Biblia ni neno la Mungu lenye uhai. Neno la Mungu ni pumzi ya Mungu aliyompulizia mwanadamu alipoumbwa pale bustani ya Edeni.
Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki. Ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema 2Timotheo 3 :16-17.
uhai wa mwanadamu umejengwa katika uhalisia wa neno la Mungu la kweli, Maisha ya mwanadamu yanaongezeka na kukua kwa sababu ya lile la neno la Mungu lilitamkwa kwa mwanadamu.
Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidi, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo                   Kumb 28:1
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.                                                     Yoshua 1:8
Kufanikiwa kwa njia yako katika Maisha yako iko katika kuisikia, kutunza kuyafanya maagizo yote ambayo Bwana, Mungu wako amekuagiza na huko kunakufanya usitawi sana.
Kusitawi kwako kupo katika kulitafakari/ meditate neno la Mungu na kulifanyia kazi katika Maisha yako.
Neno la Mungu lina uwezo wa kufanikisha Maisha ya mwanadamu
Kulisikia neno la Mungu na kuyatunza maagizo yaliyo katika neno la Mungu kunaleta baraka za Mmungu.
Kulitafakari na kuangalia kutenda sawasawa na yaliyoandikwa humo kunafanikisha njia yako na kukustawisha
Neno la Mungu lina nguvu ya kumuinua mtu kutoka kwenye hali mbaya hadi kwenye hali nzuri ya kiuchumi, kiafya, kiufahamu n.k.
Neno la Mungu lina uwezo wa kumpa mwanadamu akili na ufahamu wa kuamua mambo magumu
Tunaishi kwa sababu ya neno la Mungu.
Neno la Mungu ni jambo linalopingwa wakati wote,watu wote wasiamini, mahali pote pa uso wa nchi ni kwa sababu ya msingi kuwa hizi ni falme mbili,
Kuna wimbi kubwa sana la mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambalo linaikumba jamii ya leo, siku za leo hata vipindi vya darasani viko online na assignment zinafanyika online.
Hali hiyo hiyo iko hadi katika kanisa kila jambo liko kwa kielektroniki kuabudu, neno la Mungu hata kutoa sadaka ni online.
Mada yangu kubwa leo ni kutaka kukuonyesha kwa sehemu ndogo tu hatari iliyopo katika kutumia Biblia za kielektroniki/softcopy/software Bible
Biblia za kielektroniki ni zile biblia za simu, computer n.k ambazo wakristo wengi leo wanaweza kuzibeba kwa sababu hazina msigo mzito tofauti za kawaida ambazo kuzibeba zinahitaji nguvu ya ziada siku za leo.
Makala haya ni tafiti ndogo niliyoifanya kwa muda fulani ili kupata ufahamu juu ya jambo hili japo bado halijakamilika kwa utandani kutokana na wakati bali nimependa tushirikishane kidogo kisha tuendelee mbele zaidi.
Ufalme wa shetani siku zote haupendi kuona wala kusikia kuwa mtu aliye katika ufalme wa Mungu Jehova amefanikiwa ndio maana kila jambo linaweza likafanyika ili kuzuia na kuharibu mambo mema


Katika kizazi cha sasa tunajua kuwa maisha yetu yanaendeshwa na sayansi na teknolojia kwa sehemu kubwa. Vivyo hivyo hata ubunifu na matumizi yake kila siku yanakua ni kwa sababu ya msingi ya wakati wa kanisa tulio nao ni wakati wa kuongezeka kwa maarifa.
Tuko kwenye kipindi cha taadhari sana na uangalifu mkubwa sana
Yako mambo machache nataka nilete kwako kuhusu mada yangu ya hatari ya matumizi ya Biblia za mitandaoni.
Neno la Mungu linapokuja kwenye maisha yako inategemea sana na nguvu ya yule anayeleta hilo neno la Mungu, wengi wa wahubiri wa leo ni wale wanaotumia maarifa yao katika kutafakari neno la kweli la Mungu si kwa nguvu iliyofunuliwa kwetu na Roho mtakatifu.
Wengi wa waalimu au wahubiri wa neno hilo la Mungu ni wale wanaona kuwa njia zao au matendo yao ndio bora kuliko ya mwingine kwa maana kuwa kile anachokifanya ndio ni kizuri kuliko cha mwingine. Wengi ni wale wanaotaka kufanya ili wengine waone nini nafanya au na mimi naweza kufanya wengine waone na mimi naweza.
Hata hizo biblia zetu za kwenye simu au ku install kwenye computer na vifaa vingine kama hivyo waasisi wengi hawana ile nguvu ya Mungu ya kweli inayoweza kumbadilisha mtu bali ni kufanya ili wengine waone au kupata faida za kimtandaoni japo kweli wapo wengine ambao Mungu Jehova anawatumia kusema na maisha yetu.
§  Kutumia Biblia kwenye simu au computer au kifaa chochote chenye uwezo wa kuhifadhi Biblia haikupi nafasi ya wewe kukaa na kutafakari lile neno kwa undani
Mara nyingi matumizi yake yanakuwa ya mchanganyiko na mambo mengine mfano halisi kwenye simu utakuta unasoma Biblia huku unatuma text kwenye mitandao au mtu mwingine mambo kama hayo hayakupi bidii ya kutunza na kuyafanya yale unayoagizwa.
Wimbi kubwa la vijana hawaoni shida kwenda ibadani na kuchat katika mitandao mbalimbali ya kijamii wakiwa ibadani
Kuna siku nilihudhuria ibadani mchungaji kiongozi alitoa onyo kwa wale wote wanao chat ibadani kwa kisingizio kuwa wanatumia Biblia kwa njia ya simu.
Jambo hili linaweza kusababisha kupunguza thamani ya Mungu ndani ya mtu kwa sababu concentration kubwa iliyopo ni kwenye mitandao sio kwa Mungu
*    Kumbuka kulitafakari mchana na usiku na kutenda sawasawa na yaliyoandikwa humo kunakupa kuifanikisha njia yako na kukustawisha.
Kusikia kwa bidii kile kinachozungumzwa kwenye hilo andiko na kutunza kuyafanya yote kunakupa baraka.
Ufunuo 1 : 3 heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo ; kwa maana wakati u karibu
§  Mfumo wa ulimwengu wa giza kuamua kupoteza neno la Mungu katika maisha ya mwanadamu.
Kuna mifumo mingi inayotumika kuharibu maisha ya walioamini hasa kumfanya aendane na wakati.
Mfumo huu umeandaliwa ili kulipoteza kabisa neno la Mungu kwa mwanadamu, leo teknolojia imetusaidia kufanya mambo mengi kwa urahisi kabisa na hata kuona  kubeba Biblia  ni mzigo mzito hatimaye katika fahamu itajengeka hakuna umuhimu wa kutumia Biblia, maamuzi yatakayotokea hapo ni kuamua kuiacha kabisa na kuendelea kutumia simu zetu kama njia rahisi.
Biblia inatukumbusha kuwa kama wakristo watu tulionunuliwa kwa damu ya thamani pale msalabani inatupasa kuukomboa wakati maana ni zama za uovu.
Siku za nyuma kidogo mtu akienda ibadani anaweza kubeba Biblia na diary kwa kwa ajili ya short notice leo mkristo anaweza kwenda ibadani akiwa na simu tu kisha akatumia kama biblia na diary kwa wakati mmoja.
Kumbuka hiyo softcopy ambayo inaweza kuondolewa kabisa na kutoweka kwa hiyo ikitoweka kwenye vifaa vyako na Biblia hauna itakuleta kwenye ombwe kubwa sana.
sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; Ebrania 2 :3
Uwe mwangalifu sana na hizo software unazotumia zisije kugharimu maisha yako. Tumia neno la Mungu uhalali kabisa.
Wapendwa wangu tuliochaguliwa na Bwana tufahamu kuwa tuko kwenye nyakati za mwisho za unyakuo ni kipindi hiki ndio maarifa kila kukicha yanaongezeka  kila siku jambo jipya litokea.
Unapotumia tafsiri mbalimbali za Biblia ili kupata maana iliyokamilika usitekwe sana na mambo mengi yanayoendelea bali uwe kwenye kusudi kamili la wewe.
Jihadhari mteule uwe macho Bwana wako anakuja
Mungu na akubariki sana
joshua dwende
0719 787 952

Comments