Watu wengi huwaona wenzao ni wabaya na mtazamo huu huleta magomvi.
Ukiona kanisani kwenu kuna mtu unamchukia juu ya kile anachokifanya au umeamua kutokubali tu kile anachokifanya basi ujue unatatizo kubwa kuliko hata jipu.
Kukosa ufahamu Wa uelewa Wa nafasi ya kiroho ya mtu kwa ajili ya kanisa na nafasi ya kanisa kwa mtu.
Bila ya ufahamu namna gani uwepo wako umeunganika na utendaji wa kiungu kupitia nafasi uliyonayo itakuwa ngumu kusimamia unachoamini ili kumpa Mungu mamlaka kamili kufanya vile ambavyo havijafanywa kwa muda ili kuleta impact kwenye maisha ya waamini.
Kanisa halina nafasi kwa ajili ya mtu yeyote bali *mtu ana nafasi kwa ajili ya kanisa*.
Wanaodhani kanisa lina nafasi kwa ajili yao ndo wale ambao hugombania vyeo makanisani na kuleta chuki na makundi endapo watakosa nyadhifa hizo.
Ninaposema *mtu ana nafasi kwa ajili ya kanisani kwa ulimwengu Wa roho* ni maana fupi tu kwa kutumia nafasi aliyopewa katika ulimwengu Wa roho anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kuliko kusubiri kanisani limletee mabadiliko.
Kanisa linategemea uwepo Wa watu ili walisaidie kusudi lake likamilike.
Niende mbele kidogo kwa kusema,"kabla ya kuokolewa kwako kanisa lilikuwepo tayari na ulipopata neema ya ufahamu Wa mambo ya Kiungu ukaanza kufanya mambo ambayo yaliwasaidia wengine kukua kiimani au kuhuika kiimani,kwa mantiki ndo maana nasema kanisa halina nafasi kwa ajili ya mtu bali mtu amepewa nafasi kulifaa kanisa,maisha ya wengine yamedorola si kwa sababu wako nje ya kanisa la !hasha ni kwa sababu kuna nafasi ya mtu imeminywa haina nguvu ya kusimama na kufanya jambo la kuliinua kanisa.
Imenenwa msiache kukusanyika na mnapokusanyika inabidi *mfundishane*kule kufundishana ni kutumia nafasi uliyopewa kuelewa kitu kwa ajili ya kanisa na hakuna mahali kanisa litakufundisha bali wewe utalifundisha kanisa.
*hakuna kanisa linaloweza kukufaa bali wewe unaweza kulifaa kanisa*
We are the church makers let's make the church and not the church to make us because we have already made by Christ as body of him.
Laban nzelela
0656574760
Ftf team
Comments
Post a Comment