Hakuna kitu kizuri duniani ambacho hakikuwekwa kwa sababu wala hakuna matokeo mazuri au mabaya ya ufanyaji wa mambo ambayo yalitokea bila sababu.
Ukipewa mali nyingi leo lakini usijue kwanini umepewa haitakufaa kitu kwani yawezekana usiwe na nidhamu ya kuiendeleza hivyo inaweza ikatokea siku za usoni zikapukutika,"ikiwa laana isiyo sababu haimpati mtu,vipi kuhusu baraka isiyo sababu?
Si dua la kuku tu halimpati mwewe bali hata dua la asiye jua kwanini yuko hivyo alivyo leo halimtoi hapo ulipo.
Nyuma ya Boazi kulikomboa shamba la Elimeleki kulikua na mwanamke ambaye alijua kwanini natakiwa kuambatana na Naomi bila kumuacha kwani mbona mwenzie aliondoka baada ya kuruhusiwa kwenda kujitafutia wanaume wengine.
Ruthu kwa kujua sababu akaambatana na Naomi mpaka anafanikiwa kuchukuliwa na Boazi ili kumwinuliwa kizazi marehemu mume wake.
Kiongozi asiyejua kwanini amepewa kuongoza ni mzizi wa sumu uuao wale waongozwao na kila hazina njema.
-laban nzelela
Unataka kubaki katika nafasi?
Namna pekee ya kubaki katika nafasi ni lazima kuyafahamu haya:
1 ujue kwanini uko katika hiyo nafasi,
2:kwanini wewe na hakuwekwa mwingine.
3:wakati wako wa kuitumia kwani hata kama umezaliwa na mfalme huwezi kuwa mfalme mpaka uwe na sifa zinazotosha kukufanya mfalme mfano;uwe mtoto wa kiume na pia ukishazaliwa hivyo haimaanishi utaanza kutawala bali mpaka utakapokabidhiwa.
4:uliandaliwa?
Samweli mbele ya Mzee ya Eli,elisha mbele ya Eliya,timotheo mbele ya paulo.
5:using'ang'anie matokeo ya ufanyanyo bali ng'ang'ana na chanzo kinachokusukuma kufanya unachotamani kufanya.
Kutojua kwanini unafanya uyafanyayo ni sawa na kukalia kiti cha mbele kwenye kikao bila kukaribishwa.
bro.laban nzelela
FTF team leader.
Comments
Post a Comment