KINYUME NA ULIYOPITIA.

Wakati mwingine waweza fikiri kwa juu juu tu na kubebwa na maneno ya watu.

Hasa kwenye eneo la mahusiano kati ya jinsi ya kike na ya kiume,ukisikiliza pande zote hutupia malalamiko kwa mwenzie kwamba ndo mbaya kuliko mwingine.

Ukweli ni kwamba,"wakati wewe unalia na kusema wanaume wote walaghai,waongo au wote ni sawa"

Kuna mwenzio pia analia,"kuwa wanawake wote ni wabaya,hawafai"

Samaki mmoja akioza wote wameoza,"walisema wahenga"
Lakini kauli hii kwa sasa haiwezi kutufaa kwani tunaweza tukamtoa aliyeoza kuzuia kuoza kwa wengine(we can remove the rotten one to stop the decomposition process)

Ukiwalaumu wanawake kumbuka kuna mahali wanalaumiwa wanaume pia.

Siwezi kuacha kusafiri kwa sababu wewe umepata ajali,siwezi acha kufanya maamuzi ya kuoa au kufanya ninachotaka eti kwa kuwa kuna mtu kapatikana na madhara kutokana na kuoa au kufanya biashara.

#let the nature speak.

Comments